Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kudungua ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 na kulazimisha ndege ya RQ-4 pamoja na ndege ya kivita ya F-35 kuondoka katika anga ya Iran baada ya kujibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga. IRGC imeonya kuwa uvunjaji wowote wa usitishaji mapigano utakabiliwa na majibu makali ya kulipiza kisasi.
Maafisa wa jeshi nchini Uingereza wamekiri kuhusika katika mauaji ya watoto nchini Afghanistan na kusisitiza kuwa: mauaji hayo ya nje ya mfumo wa sheria yalitekelezwa, na huenda haya ni sehemu ndogo tu ya kile kilichotokea!