30 Machi 2025 - 13:54
Kulaani Ukandamizaji na Mauaji ya watu wa Nigeria Katika Siku ya Al-Quds | Moto wa Mwamko wa Kiislamu Hautazimika

Baraza la Uratibu wa Tabligh za Kiislamu, limelaani ukandamizaji wa Maandamano ya Siku ya Quds Duniani nchini Nigeria, na limetangaza kuwa: Jinai hizo za kipofu zitazidisha azma ya Mataifa ya Kiislamu kukabiliana ipasavyo na mfumo wa ukoloni na uistikbari.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Baraza la Kuratibu Tabligh za Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kuwa: Kukandamizwa kwa kumwagwa damu za waandamanaji wa amani katika maandamano ya amani ya Siku ya Quds Duniani nchini Nigeria na kuuawa Shahidi Waislamu 18 kwa dhulma tena wakiwa wamefunga Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kunaonyesha hofu ya utawala huo juu ya mwamko wa Umma wa Kiislamu na Msimamo wa kistratijia wa Siku ya Mwenyezi Mungu (Yaumullah) katika Siku ya Quds.

Baraza hili limeongeza kuwa: Maadui wa Uislamu ambao wameelewa umuhimu wa Siku ya Quds kuwa kiini na kitovu cha kukabiliana na uvamizi na ukoloni, safari hii pia walijaribu kuzima moto wa Mwamko wa Kiislamu kwa kutumia vurugu za wazi na ukandamizaji wa kikatili. Bila ya kujua kwamba damu iliyomwagwa kinyume na Haki ya watu waliofunga Saumu katika nchi za Nigeria, Gaza na Lebanon itapanuliwa katika mstari mmoja na itakuwa na taathira mara dufu na zaidi katika njia ya kutokomeza ukatili dhulma na uhalifu.

Baraza la Uratibu wa Tablighi za Kiislamu sambamba na kulaani vikali jinai hiyo na kutangaza mshikamano wao kwa watu wa Taifa linalodhulumiwa la Nigeria, linasisitiza kuwa, njia bora ya ukombozi wa Jerusalem (Quds) itaendelea kwa nia thabiti zaidi kuliko huko nyuma. Damu ya Mashahidi wa Nigeria, kama kiungo chenye kuendelea katika mlolongo wa Upinzani (Muqawamah), ilifanya eneo hili kuwa na nguvu zaidi na kuthibitisha kwamba kuadhimisha Siku ya Quds Dunia si tukio la mara moja tu, bali ni mkakati endelevu dhidi ya utawala haram na mfumo wa uvamizi.

Ikumbukwe kuwa siku ya Ijumaa inayosadifiana na Siku ya Quds Duniani, makumi ya wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria waliandamana kwa kuonyesha mshikamano wao na Palestina. Lakini ghafla, mzozo mkali kati ya vikosi vya Polisi ulizuka na kuanza.

Vikosi vya usalama vya Nigeria vilizidi kutumia nguvu, zikiwemo risasi za moto ili kuzima maandamano hayo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha