saini
-
Kiongozi wa Iran: Ukiukaji wa Marekani unathibitisha saini yake haina thamani; Iran ina masomo yasiyosahaulika kwa adui
Katika ujumbe kuhusu kuaga kwa kishujaa kwa Kiongozi shahidi wa Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Mojtaba Khameni amesema kuwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Marekani wa makubaliano yaliyosainiwa kati ya marais wa Iran na Marekani umeonyesha tena kuwa saini ya rais wa Marekani haina thamani. Amesema pia kuwa Iran na mhimili wa muqawama wana masomo yasiyosahaulika kwa adui, kama ilivyoonekana kupitia ujasiri wa wapiganaji na uhodari wa wananchi wa maeneo ya kusini.
-
Kiongozi wa Mapinduzi Atoa Ujumbe kwa Wairan Kuhusu Makubaliano kati ya Iran na Marekani
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema aliruhusu kutiwa saini kwa hati ya makubaliano kati ya Iran na Marekani baada ya kupokea dhamana kutoka kwa Rais wa Iran kwamba haki za wananchi wa Iran na Kambi ya Muqawama zitalindwa, huku akisisitiza kuwa mazungumzo ya baadaye hayatamaanisha kujisalimisha kwa matakwa ya Marekani.
-
Iran Yatangaza Rasmi Kufikiwa kwa Rasimu ya Mwisho ya Makubaliano na Marekani; Ijumaa Kutia Saini
Iran imetangaza rasmi kwa mara ya kwanza kufikiwa kwa rasimu ya mwisho ya makubaliano na Marekani, huku Ijumaa ikitajwa kuwa siku ya kutiwa saini; wakati huo huo, wachambuzi wanaeleza kuwa usitishaji wa mapigano nchini Lebanon, endapo Israel itautekeleza, ni matokeo ya msimamo wa Iran wa kujumuisha suala la Lebanon katika makubaliano hayo na ustahimilivu wa Muqawama katika medani ya mapambano.
-
Mkataba wa mabilioni kadhaa ya dola wa Israel kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa ngao ya Chuma (Iron Dome)
Wizara ya Ulinzi ya Israel imetiliana saini mkataba mkubwa na Kampuni ya Rafael ili kuongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa makombora ya kukinga ya mfumo wa Iron Dome (Gombo la Chuma).