Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amesema Baraza la Usalama linapaswa kuunga mkono diplomasia na kuepuka hatua zinazoweza kuchochea mvutano au kudhoofisha mazungumzo yanayoendelea.
Kiongozi wa chama cha Majlis Ittehad-ul-Muslimeen nchini India, akijibu mzozo ulioibuka kutokana na mabango yenye maandishi “Nampenda Muhammad” katika jimbo la Uttar Pradesh, ameishutumu serikali ya India na viongozi wa eneo hilo kwa kuweka vizuizi vya kibaguzi na vya upendeleo.