Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anatarajiwa kuzungumza kupitia televisheni ya Iran kuhusu utendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Brigedia Jenerali Mohbi amesema Iran itaendelea na mapambano hadi kufikia ushindi wa mwisho, akisisitiza kuwa waandishi wa habari walikuwa na nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa ushindi, kuimarisha utamaduni wa upinzani na kudumisha umoja wa wananchi.
Mjumbe wa zamani wa Kamati ya Usalama na Ulinzi ya Bunge la Iraq amesema kuwa Hashd al-Shaabi (Jeshi la Wananchi wa Iraq) ni mstari mwekundu kwao, kwani ni mali ya watu wote wa Iraq na linawakilisha makabila na madhehebu yote nchini humo.