Ubalozi wa Iran nchini Uingereza umejibu upotoshaji wa vyombo vya habari vya Kiingereza kuhusu wakimbizi wa Afghanistan walioko Iran, na umepinga madai ya uongo yaliyotolewa na vyombo hivyo vya habari vya Kiingereza kwamba kuna uwezekano wa kufukuzwa kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan kwenda katika nchi jirani.
Serikali ya Taliban imejibu kauli za Donald Trump kuhusu kurejesha kambi ya Bagram kwa kusema kuwa uwepo wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan ni jambo lisilowezekana kabisa.