Main Title
18 Mei 2024
Iran: Marekani na Magharibi hazisiti kukiuka sheria za kimataifa
Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameasema kuwa sheria za kimataifa zinakabiliwa na udhaifu wa dhamana ya utekelezaji na kusisitiza kuwa: Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinakubali sheria za kimataifa kiubaguzi na hazisiti kukanyaga haki hizo kwa kutumia visingizo vya kisiasa.
18 Mei 2024
Bagheri: Iran na Russia zimegeuza vikwazo vya Marekani kuwa fursa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika Mkutano wa "Russia na Ulimwengu wa Kiislamu" kwamba: Vikwazo vya Marekani vimegeuzwa kuwa fursa kwa busara na viongozi wa Tehran na Moscow.
18 Mei 2024
Hamas: Asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni wameuawa katika mashambulizi ya Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambao unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo, yameuwa asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao walikuwa wakishikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa mwezi Oktoba mwaka jana.
18 Mei 2024
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Utawala wa Kizayuni umeshindwa huko Gaza
Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesema: Utawala wa Kizayuni wa Israel haujafanikiwa lolote katika mashambulizi yake huko Gaza isipokuwa kushindwa.
18 Mei 2024
Sami Abu Zuhri: Marekani ni mshirika wa jinai dhidi ya taifa la Palestina
Sami Abu Zuhri, Kiiongozii wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiiislamu ya Palestina HAMAS nje ya nchi amesema kuwa, serikali ya Marekani ni mshirika wa vita dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
18 Mei 2024
Wapalestina: Tuko tayari kwa 'vita vya muda mrefu' Rafah
Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) limetangaza kuwa Wapalestina wako tayari kwa vita vya muda mrefu, na kuahidi kukabiliana na uvamizi wa nchi kavu wa Israel dhidi ya Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza na kwingineko.
17 Mei 2024
Italia yaitaka Israel isitishe operesheni za kijeshi Rafah
Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomesha operesheni zake za kijeshi katika mji wa Rafah, wa kusini mwa Ukanda wa Gaza.
17 Mei 2024
Mafanikio ya uvumbuzi wa wanawake wa Iran katika nyanja mbalimbali
Ingawa bado kuna pengo kubwa kati ya wavumbuzi wanawake na wanaume duniani lakini viashiria vilivyopo vinaonyesha kuwa juhudi zinazofanywa na wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuziba pengo hilo zinaendelea kwa kasi kubwa.
17 Mei 2024
Iran yaikataa taarifa 'isiyokubalika' ya Arab League kuhusu visiwa vyake vitatu vilivyoko Ghuba ya Uajemi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetupilia mbali kauli "isiyo na msingi" na "isiyokubalika" iliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusiana na visiwa vitatu vya Abu Musa na Tunb Kubwa na Ndogo vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa visiwa hivyo vitabaki kuwa milki ya Iran.
17 Mei 2024
Viongozi wa Kiarabu waondoka Bahrain bila ya msimamo wowote wa kuiadhibu Israel kwa jinai za Ghaza
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito katika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama uliofanyika nchini Bahrain wa kuundwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina na kuitishwa mkutano wa kimataifa wa amani, lakini imeshindwa kuidhinisha hatua yoyote ya kuuadhibu kiuchumi na kisiasa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mauaji ya kimbari unayoendelea kufanya dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
17 Mei 2024
"Kuna haja ya kuitetea Gaza katika Hija ya mwaka huu"
Rais wa Chuo cha Da'awa ya Kiislamu cha Lebanon amesema ibada ya Hija ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee wakati huu ambapo Wazayuni wanaendelea kumwaga damu za Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa, "Kuna haja ya kuitetea Gaza katika Hija ya mwaka huu."
17 Mei 2024
HAMAS: Mashambulio ya Israel yameua 70% ya mateka wa Kizayuni
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, unaokabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo ghasibu, yameua asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao wanashikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu ilipotekelezwa operesheni ya mwezi Oktoba ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
17 Mei 2024
Mawaziri 13 wa Mambo ya Nje wakiwemo 6 wa G7 waitaka Israel isitishe uvamizi wa ardhini wa Rafah
Shirika la habari la DPA la Ujerumani limeripoti kuwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi 13 wametia saini barua ya kuuonya na kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa ardhini katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza na kuruhusu misaada zaidi kuwafikia Wapalestina.
17 Mei 2024
Wazayuni washambulia misafara ya misaada ya kibinadamu huko Gaza
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakishambulia malori yanayobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza karibu na mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
17 Mei 2024
Afisa Myahudi katika serikali ya Biden ajiuzulu kulalamikia mauaji ya kimbari ya Ghaza
Lily Greenberg Call, msaidizi maalumu wa mkuu wa wafanyakazi katika Idara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Marekani amekuwa mteuliwa wa kwanza wa kisiasa wa Kiyahudi kujiuzulu hadharani akipinga uungaji mkono wa Washington kwa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika katika Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro.
17 Mei 2024
Ireland kuitambua rasmi nchi huru ya Palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland amesema kuwa, mnamo siku chache zijazo, Dublin itaitambua rasmi nchi huru ya Palestina.
15 Mei 2024
Katibu Mkuu wa UN alaani mauaji ya wafanyakazi wa afya huko Rafah
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amelaani mauaji na kujeruhiwa kwa maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza.
15 Mei 2024
IDMC: Kuna ongezeko kubwa la ukimbizi wa ndani unaosababishwa na migogoro duniani
Ripoti mpya ya Kituo cha Ufuatiliaji wa Ukimbizi wa Ndani (IDMC) inaonyesha kuwa migogoro na ghasia duniani zimesababisha ongezeko lisilo na kifani la idadi ya wakimbizi wa ndani kufikia mwisho wa 2023.
15 Mei 2024
Uchunguzi wa Independent: Biden anahusika katika mateso ya njaa ya watu wa Gaza
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Uingereza la The Independent unasema kuwa, Rais wa Marekani, Joe Biden, anahusika katika baa la njaa linalowatesa raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
15 Mei 2024
Iran: Haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja
Ali Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja kwani zote zinakiuka pakubwa haki za binadamu dhidi ya mateka na wafungwa, moja huko Negev na nyingine huko Guantanamo na Abu Ghraib.