Main Title
14 Mei 2024
Askari 1,400 wa Ukraine wauawa Donetsk, Luhansk ndani ya saa 24
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza habari ya kuuawa wanajeshi 1,400 wa Ukraine katika muda wa saa 24 katika maeneo ya mashariki ya Luhansk na Donetsk, yaliyojitangazia uhuru mwaka 2014, baada ya kutokea mapinduzi nchini Ukraine.
14 Mei 2024
FIFA kupiga kura ya kuamua kuifutia uanachama Israel kutokana na jinai zake Gaza
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mwezi huu linatarajiwa kupiga kura ya kuamua kuifutia uanchama Israel au la kutokana na kutenda jinai kubwa dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
14 Mei 2024
UNICEF yataka kukomeshwa mauaji ya watoto yanayofanywa na Israel Gaza
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetoa mwito wa kukomeshwa mauaji ya kiholela dhidi ya Wapalestina, hasa watoto wadogo katika Ukanda wa Gaza.
14 Mei 2024
Balozi wa Yemen nchini Iran: Mkutano wa Tehran utaleta maelewano kati ya Iran na Waarabu
Balozi wa Yemen nchini Iran amesema kuwa Mkutano wa Mazungumzo ya Iran na Waarabu uliofanyika mjini Tehran chini ya anwani "Kwa ajili ya Ushirikiano na Maelewano" utaliimarisha taifa la Palestina na kuboresha maelewano kati ya Iran, Waarabu na nchi mbalimbali.
14 Mei 2024
Familia za wanajeshi waliouawa zamshambulia Waziri wa Usalama wa Israel
Familia za wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliouawa vitani Ukanda wa Gaza zimemshambulia Itamar Ben- Gvir Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni.
14 Mei 2024
Nasrullah: Wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya Gaza
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema wanajeshi 1,500 wa Israel wameuawa tangu kuanza vita vya utawala huo haramu dhidi ya Gaza, jambo ambalo limeyalazimu makundi ya muqawama katika eneo la Magharibi mwa Asia, ikiwemo Hizbullah, kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel ili kuilazimisha kukomesha vita hivyo.
14 Mei 2024
Sababu za kushindwa mazungumzo ya kusitishwa vita vya Gaza
Khalil al-Hayya, Naibu Mkuu wa Hamas katika Ukanda wa Gaza, amefafanua jinsi utawala wa Kizayuni wa Israel ulivyovuruga mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na kubadilishana mateka.
14 Mei 2024
Yemen yaonya inaweza kulenga shabaha za adui 'ambazo hawezi hata kuzifikiria'
Jeshi la Yemen limeonya kuwa huenda likazidisha mashambulizi yake ya kuiunga mkono Palestina iwapo utawala wa Israel utaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.
14 Mei 2024
Amir wa Qatar na Waziri Mkuu wa Malaysia wajadili uhusiano wa pande mbili na hali ya Gaza
Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani amekutana na kufanya mazungumzo na Anwar Ibrahim Waziri Mkuu wa Malaysia katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha. Waziri Mkuu wa Malaysia yuko nchini Qatar kwa ziara ya siku tatu.
14 Mei 2024
Makumi ya Wapalestina wauawa katika hujuma za Israel Gaza
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimefanya mashambulizi mapya ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza na kuua shahidi makumi ya Wapalestina, wakiwemo watoto wadogo na wanawake.
13 Mei 2024
Iran: Amani ya Asia Magharibi inategemea kupokonywa silaha Israel
Iran inasema kuimaishwa amani kamili na ya kweli, utulivu na usalama katika eneo la Asia Magharibi kunategemea kupokonywa silaha kwa utawala ghasibu wa Israel na kukomeshwa kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
13 Mei 2024
Wairani waanza safari ya kulekea ardhi ya Wahy kwa ajili ya ibada ya Hija
Misafara ya kwanza ya Wairani wanaoelekea katika ardhi ya wahyi kwa ajili ya ibada ya Hija imeondoka nchini mapema leo.
13 Mei 2024
Azma ya Iran ya kuimarisha ushirikiano na nchi za kieneo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir Abdollahian amesisitiza katika kikao cha mkutano wa tatu wa Mazungumzo kati ya Iran na Waarabu uliopewa jina la "Kwa Ajili ya Ushirikiano na Maingiliano" kwamba Iran imeazimia kukuza na kuzidisha maelewano na ushirikiano na nchi za eneo la Magharibi mwa Asia.
13 Mei 2024
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu atembelea Maonyesho ya Vitabu ya Tehran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu mjini Tehran
13 Mei 2024
Vita vya Gaza na kuibuka mzozo kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umetangaza kuwa, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni hana mamlaka ya kisheria ya kuamua kuhusu hatima ya uongozi na uendeshaji wa Gaza baada ya vita.
13 Mei 2024
UNRWA: Akiba ya chakula kusini mwa Ghaza inakaribia kwisha kabisa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa indhari kwamba, ikiwa misaada ya kibinadamu haitaingizwa Ghaza, hakutakuwa na chakula chochote cha kuwagaia wakazi wa eneo hilo lililowekewa mzingiro.
13 Mei 2024
Maandamano ya kuunga mkono Palestina na Ghaza yaendelea katika miji mbalimbali duniani
Watu wa miji tofauti katika nchi mbalimbali duniani, kwa mara nyingine wamemiminika mabarabarani wakiandamana kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina hususan wa Ukanda wa Ghaza na kulaani jinai za mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo.
13 Mei 2024
Uingereza yatupilia mbali miito ya kuitaka isitishe uuzaji silaha kwa Israel
Serikali ya Uingereza imekataa miito ya kuitaka ifuate mwelekeo ulioonyeshwa na Marekani wa kutishia kusitisha baadhi ya mauzo ya silaha kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ikiwa utafanya operesheni kubwa ya ardhini katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Ghaza unaowapa hifadhi wakimbizi Wapalestina wapatao milioni moja na laki nne.
13 Mei 2024
Al-Nakhalah: Muqawama ndilo chaguo bora zaidi la kukomesha kukaliwa kwa mabavu Palestina
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema, Muqawama ndilo chaguo bora zaidi la kukomesha kukaliwa ardhi ya Palestina kwa mabavu.
13 Mei 2024
Ripoti: Wahudumu wa afya 500 wameuawa katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Israel yameua mamia ya madaktari na wahudumu wa afya katika eneo hilo linalozingirwa.