Main Title
13 Mei 2024
Hizbullah yazindua kombora jipya katika shambulio dhidi jeshi la Israel
Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imetumia kwa mara ya kwanza kombora zito kushambulia eneo la kijeshi la Israel katika sehemu ya kaskazini ya maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 kwa ajili ya kulipiza kisasi vita vya umwagaji damu vya Israel dhidi ya Gaza.
13 Mei 2024
Mfumo wa huduma ya afya wa Gaza unakaribia kusambaratika kabisa
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, ambayo inaendelea kustahamili vita vya mauaji ya kimbari vinavyotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika eneo hilo imeonya kuhusu kusambaratika kabisa mfumo mzima wa afya katika eneo hilo.
12 Mei 2024
Polisi wa Uswidi washambulia waandamanaji wanaounga mkono Palestina katika fainali ya Eurovision
Polisi wa Uswidi wamewashambulia waandamanaji wanaounga mkono Palestina wanaopinga ushiriki wa utawala wa Israel katika Mashindano ya Muziki ya Eurovision kusini mwa Uswidi.
12 Mei 2024
Kukanushwa madai ya Israeli na serikali ya Uturuki
Kufuatia kufichuliwa kufutwa vikwazo vya kiuchumi na kibiashara vya Uturuki dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Israel, mivutano kati ya pande hizo mbili imeshtadi katika vyombo vya habari vya eneo na kimataifa.
12 Mei 2024
Rais wa Colombia: Netanyahu ataingia katika historia kama mhalifu wa mauaji ya kimbari
Rais Gustavo Petro wa Colombia amemshambulia kwa maneno Waziri Mkuu wa utawala wa Israel Benjamin Netanyahu akisema historia itamuandika kama mhalifu wa mauaji ya kimbari.
12 Mei 2024
Borrel asema uhamisho hauvumiliki; aikosoa Israel kwa kuwahamisha kwa lazima Wapalestina katika mji wa Rafah
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amelaani na kuitaja kuwa isiyovumilika hatua ya utawal wa Israel ya kuwaondoa kwa lazima raia wa Kipalestina katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. Utawala wa kizayuni umechukua hatua hii huku ukijiandaa kuanzisha mashambulizi makubwa ya ardhini katika mji huo.
12 Mei 2024
Iran: Israel haijawahi kutengwa kiasi hiki katika historia yake bandia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha rasimu ya azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo na kusema kuwa, utawala haramu wa Israel haujawahi kutengwa kwa kiwango kikubwa kama cha sasa katika historia yake bandia.
12 Mei 2024
IRGC: Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilikuwa jibu la Iran kwa makosa ya Israel
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya Iran ilikuwa hatua ya wakati muafaka ya kutoa adhabu kwa kosa la kistratijia la utawala wa Kizayuni wa Israel la kushambulia jengo la kidiplomasia la Jamhuri ya Kiislamu nchini Syria.
12 Mei 2024
Balozi wa Iran nchini Iraq: Usalama wa taifa ni mstari mwekundu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Balozi wa Iran nchini Iraq ameashiria uhusiano mkubwa na wa kistratejia kati ya nchi mbili na kusema: Usalama wa taifa ni mstari mwekundu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
12 Mei 2024
Afisa wa Hamas: Muqawama wa Gaza umeweza kukabiliana kwa mafanikio na vita vya dunia
Sami Abu Zuhri, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kwamba Muqawama na mapambano ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kukabiliana na "vita vya kimataifa," na nchi zilizoifadhili Israel sasa zinaanza kusitisha uungaji mkono wao kwa utawala huo.
12 Mei 2024
Hizbullah yatekeleza mashambulizi ya mizinga na droni dhidi ya ngome za Israel
Wapiganaji wa harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, wamefanya mashambulizi kadhaa ya kijeshi kwa kutumia ndege zisizo na rubani (droni) na mizinga dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel kaskazini mwa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ukanda wa Gaza.
12 Mei 2024
Mtangazaji nguli wa soka Uingereza: Yanayojiri Gaza ni mabaya zaidi kuliko yote niliyoshuhudia maishani
Mtangazaji nguli wa soka wa Uingereza, Gary Lineker ameema mauaji yanayofanywa na jeshi la Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina ndio mabaya zaidi aliyowahi kushuhudia katika kipindi chote cha maisha yake.
12 Mei 2024
Jihad Islami: Israel haitatimiza malengo yake kwa mashambulizi ya kikatili ya Gaza
Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imesema Israel haitaweza kufikia malengo yake katika Ukanda wa Gaza kupitia mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Wapalestina.
11 Mei 2024
Rais wa Colombia aitaka ICC itoe waranti wa kukamatwa Netanyahu
Rais Gustavo Petro wa Colombia ameiasa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutoa waranti wa kumtia nguvuni Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita katika Ukanda wa Gaza.
11 Mei 2024
Kuidhinishwa rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) hatimaye limeipigia kura ya ndio rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika umoja huo baada ya Marekani kukwamisha suala hilo kwa miaka kadhaa.
11 Mei 2024
WHO: Mkataba wa majanga wakwama kuidhinishwa
Nchi 194 wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) zimeshindwa kuafikiana juu ya mkataba uliotafutwa kwa muda mrefu wa kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na majanga.
11 Mei 2024
Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Mafuta na Gesi ya Tehran
Maonyesho ya 28 ya Kimataifa ya Mafuta, Gesi, Viwanda vya Usafishaji na Petrokemikali ya Iran yalianza Jumatano wiki hii mjini Tehran kwa kushirikisha zaidi ya makampuni 1,500 ya ndani na 250 ya kigeni.
11 Mei 2024
Iran: Kuipa uanachama Palestina, ni hatua ya kwanza ya kukabiliana na dhulma
Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Tehran inakaribisha hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo.
11 Mei 2024
Nasser Kan'ani: Jeshi la SEPAH ni mbeba bendera ya kupambana na ugaidi
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, mpango wa Bunge la Kanada wa kuwatangaza Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa ni magaidi ni hatua isiyo ya busara, ya kiuadui na kinyume na viwango na kanuni zinazokubalika za sheria za kimataifa.
11 Mei 2024
Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yakwama, wajumbe wa Hamas na Israe waondoka Cairo
Mazungumzo yaliyokuwa na lengo la kuhitimisha vita vya Gaza yaliyokuwa yakifanyika huko Cairo Misri yamekwama na pande mbili zimeshindwa kufikia makubaliano.