Hujjatul Islam Abutorabi-Fard ameendelea kusisitiza kuwa: "Tuko katika hatua ya mwisho ya mazishi yenye heshima na yenye kuleta nguvu ya kiongozi wa muqawama, kamanda shujaa, mwanazuoni na mtu madhubuti wa Hizbullah. Shakhsia huyu alikuwa bega imara la mapinduzi na umma, pamoja na mhimili wa muqawama, akiwa na sifa za kipekee. Sifa ambazo Kiongozi Muadhamu anasema kuwa kweli zimeuletea Uislamu heshima. Heshima hii ni matunda ya imani na matendo mema aliyoyafanya. Alikuwa mtu mwenye heshima na mjumbe wa heshima kwa umma wa Kiislamu."
Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo Tehran ameendelea kusema: "Shahidi Nasrallah alikuwa mtu mwenye busara na asiye na kifani ambaye kwa miongo kadhaa aliongoza muqawama na Hizbullah, akifungua njia ya kuunda nguvu nyingine katika ulimwengu wa Kiislamu na pia kuunganisha safu za mhimili wa muqawama. Leo, tunashuhudia nguvu ya muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon, uimara wa Yemen, ushindi wa wapiganaji wa Gaza na msimamo thabiti wa wanamuqawama wa ulimwengu wa Kiislamu."
342/
