Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Idara ya Habari ya Serikali ya Palestina huko Gaza kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake imesema: "Katika vita vya Gaza, wanawake 13,901 wamefanywa wajane na akina mama 17,000 wamepoteza watoto wao."
Taarifa hiyo imesema, wanawake na wasichana 2,000 wa Kipalestina wamepata ulemavu wa kudumu kutokana na mashambulizii ya kinyama ya utawala wa Israel, na katika awamu ya hivi karibuni, makumi ya wanawake wa Kipalestina wametiwa mbaroni na kuteswa ndani ya jela za Israel.
Ofisi hiyo imeeleza kuwa wanawake wa Gaza wanakabiliwa na kifo cha polepole kutokana na kuzingirwa, ukosefu wa suhuula za afya na kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu kuingia katika eneo hilo al Palestina.
Ripoiti zinasema: Vita na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Gaza yamekuwa na taathira kubwa zaidi kwa wanawake na watoto na hivyo kuwatengenezea mazingira magumu.
Dunia leo tarehe 8 Machi inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiendelea kupaza sauti za kulaani ukatili unaofanywa na Israel dhidi ya wanawake wa Palestina.
/342
Your Comment