9 Machi 2025 - 22:10
Source: Parstoday
Mkutano wa Jeddah; licha ya kukamilisha lakini ni zaidi ya mkutano wa Cairo

Kufanyika mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Kiislamu huko Jeddah mara baada ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa Mambo ya Nje na Wakuu wa Nchi za Kiarabu huko Cairo, Misri kunaonyesha ushirikiano wa pamoja wa Ulimwengu wa Kiislamu katika kukabiliana na mpango wa kuwafukuza kwa nguvu wakazi wa Ukanda wa Gaza na wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Alhamisi alasiri aliwasili Jeddah nchini Saudi Arabia akiongoza ujumbe wa nchi hii kwa shabaha ya kushiriki katika mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC). Hii ni ziara ya pili ya Sayyid Abbas Araqchi nchini Saudia. 

Mkutano wa Jeddah; licha ya kukamilisha lakini ni zaidi ya mkutano wa Cairo

Mkuu wa chombo cha diplomasia wa Iran mwezi Oktoba mwaka jana pia alielekea mjini Riyadh akiendelea na ziara yake ya kikanda kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa Saudi Arabia kuhusu hali ya mambo ya Gaza na Lebanon; ambapo alikuwa na mazungumzo na Faisal bin Farhan Waziri wa Mambo ya Nje na Muhammad bin Salman Mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo.  

Sambamba na kushiriki katika mkutano wa Jeddah na kutoa hotuba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Hossein Ibrahim Taha Katibu Mku uwa OIC na baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa jumuiya ya OIC. 

Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu umefanyika ili kutoa msukumo na kuuhamasisha Ulimwengu wa Kiislamu kukabiliana barabara na njama zozote za kuwahamisha kwa nguvu wananchi wa Palestina kutoka Ukanda Gaza, ambazo bila shaka leo hii  zimeenea hadi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huku utawala wa Kizayuni pia ukiliweka katika ajenda yake ya kazi mchakato huu unaoongezeka wa kutaka kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Kipalestina wa Ukingo wa Magharibi.

Sayyid Abbas Araqchi ameanzisha harakati kubwa ili kuratibu na kuleta sauti moja miongoni mwa nchi za Waislamu dhidi ya mpango huu tajwa tangu Rais wa Marekani aibue tena mkakati huu wa Wazayuni wa kutaka kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Ukanda wa Gaza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika muda wa wiki moja amekuwa akiwasiliana kwa simu na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje wa Tunisia, Misri, Uturuki, Pakistan, Gambia, Malyasia, Algeria na Saudi Arabia.  

Ajenda kuu ya mashauriano hayo ya simu yalikuwa ni kuhusu upinzani wa wazi wa Tehran kwa mpango wa kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Gaza na haja ya kufanyika mkutano wa dharura wa OIC kwa ajili ya kufuatilia kadhia hii. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesisitiza katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu udharura wa Umma wa Kiislamu kuwa na msimamo wa pamoja ili kusambaratisha na kuzima njama hii hatari ya Marekani na Wazayuni na kusisitiza kuwa: Mpango wa kuwafukuza kwa nguvu Wapalestina kutoka Gaza si tu ni jinai kubwa na inayoshabihiana na "mauaji ya kimbari", bali una taathira hatari kwa uthabiti na usalama wa eneo na ulimwengu kwa ujumla;  na kwamba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu inapasa kuitisha haraka iwezekanavyo mkutano wa dharua wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa OIC ili kuchukua uamuzi madhubuti na chanya wa kutetea haki za wananchi wa Palestina. 

Kufuatia harakati hizi za kidiplomasia, iliamuliwa kufanyika kikao cha dharura cha jumuiya ya OIC kwa pendekezo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Ismail Baqaei Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Jumatano iliyopita alisema kuhusu muhtawa na ajenda ya mkutano wa OIC kwamba: Madhumuni ya ombi la kufanyika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ni kuitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kutilia maanani suala hili kwa kuwa ndio jumuiya muhimu zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu mkabala wa suala ambalo ndilo kadhia na changamoto kuu inayoisibu  jamii na nchi za Kiislamu; na hilo si suala jingine isipokuwa ni indhari kuhusu kuendelea hatari ya maangamizi ya kizazi ya wananchi wa Palestina khususan huko Ukanda wa Gaza.

Mkutano wa Jeddah; licha ya kukamilisha lakini ni zaidi ya mkutano wa Cairo

Mkutano wa Jeddah umefanyika baada ya mkutano wa dharura wa karibuni wa viongozi wa Kiarabu huko Misri, ambapo wakuu hao wa Kiarabu wameadili na kushauriana kuhusu matukio ya Palestina na njia ya kutetea na kuwasaidia wananchi wa Palestina dhidi ya mpango wa Trump wa kuwahamisha kwa nguvu katika ardhi yao. 

Mpango wa dola bilioni 53 ulioidhinishwa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (ArabLeague) utaruhusu takriban Wapalestina milioni 2 wakazi wa Gaza kusalia katika ardhi yao. Ujenzi mpya wa Gaza umetabiriwa kuendelea hadi mwaka 2030 bila ya kuhamishwa jamii ya ukanda huo. Mpango wa Waarabu wa kuijenga upya Gaza ni jibu mkabala wa mpango uliopendekezwa na Marekani na Israel kuhusu Gaza ambapo kupitia mpango huo ilipangwa kuwa wakazi karibu karibu milioni mbili wafurushwe katika ukanda huo kupitia kivuko cha mpakani cha Karem Abu Salem na kisha kupitia bandari ya Ashdod na uwanja wa Ramon. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha