Katika sehemu moja ya makala yake hiyo limeandika: Mtazamo wa rais wa Marekani, Donald Trump ni kwamba mshindi lazima awe mmoja tu na waliobakia imma wawe wasaidizi au wapinzani wa shujaa na mshindi huyo.
Katika makala hiyo ya kiuchambuzi gazeti la The Guardia aidha limeandika: Kwenye kipindi cha wiki sita zilizopita, viongozi wengine wa dunia, watu ambao wenyewe wanatambua kwamba tawala zao hazikutoka kwa Mungu na wala hazikuzaliwa na studio ya televisheni (kama Trump), wamekuwa waangalifu sana wanapofika kwenye masuala yanayomuhusu rais wa Marekani.
Amma kuhusu tabia ya Trump ya kujifanya mbabe, gazeti hilo limegusia mkasa wa hivi karibuni wa kudhalilishwa rais wa Ukraine katika Ikulu ya Marekani wakati Trump na makamu wake, DJ Vance walipomuweka "kiti moto" Volodymyr Zelenskyy na kuandika: "Trump, ambaye muda wote alikuwa anajaribu kujionyesha ni mtu mwenye nguvu, alidhihirisha haraka uhakika wake wa kujifanya mbabe lakini kumbe ni dhaifu."
Kwa mujibu wa makala hiyo ya karibuni kabisa ya gazeti la The Guardian, vitendo vya Trump vimeharibu kabisa maadili (yanayodaiwa) kulindwa na Marekani, ikiwa ni pamoja na eti kupigania usawa, kutoa fursa sawa, kukubalika mbele ya watu wote, kupinga unyonyaji wa kukuza vipaji bora. Muda wote Marekani inapigia upatu mambo hayo, lakini Trump hivi sasa amethibitisha uhalisia wa mambo ambao ni kinyume kabisa na madai hayo ya Marekani.
342/
Your Comment