Efrat Livni, mwandishi wa New York Times ameripoti kuwa Wakristo wa Kiinjili wanatafuta njia ya kunyakua ardhi ya Palestina ya Ukingo wa Magharibi ambayo kimataifa imetengwa kwa ajili ya taifa la baadaye la Palestina.
New York Times limeongeza kuwa wafuasi mashuhuri wa Evangelisti wa Doland Trump wanapenda kuzuru Israel na kutia saini maombi ya kutaka kutwaliwa eneo la Ukingo wa Magharibi, na wanahamasisha uungaji mkono katika Bunge la Marekani kwa matakwa yao.
Gazeti hilo la Marekani limeripoti kuwa, viongozi wa Evangelisti ni sehemu ya vuguvugu la Wazayuni wa Kikristo na wanaamini kwamba ardhi hiyo ya Palestina ilitolewa kwa Wayahudi katika Biblia.
Kwa mujibu wa New York Times, mojawapo ya makundi mashuhuri zaidi yanayofanya kazi katika mfumo huu ni kundi la American Christian Leaders for Israel (ACLI), ambalo linapinga mashinikizo ya aina yoyote ya Marekani kwa Israel.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa,wafuasi wa Kiinjilisti wanaomuunga mkono Trump wanatumai kwamba ataunga mkono mpango wa kunyakuliwa Ukingo wa Magharibi ili kukomesha mjadala wowote kuhusu kuundwa taifa la Palestina katika siku zijazo.
New York Times limesema kuwa baadhi ya maamuzi ya Trump yametekeleza matakwa ya Wakristo wa Kiinjilisti, kwani mwezi uliopita aliunga mkono mpango wa kuhamishwa Wapalestina kwa nguvu kutoka Ukanda wa Gaza, na mnamo Januari alifuta amri ya utendaji ya rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, iliyoruhusu kuwekewa vikwazo walowezi wa Israel katika ardhi ya Palestina ya katika Ukingo wa Magharibi.
Vilevile Trump amewateua wanachama wa vuguvugu hilo la Wakristo wenye fikra za Kizayuni kujaza nyadhifa muhimu katika utawala wake, akiwemo Paula White Kane kama mshauri wa Ofisi mpya ya Imani ndani ya White House.
342/*
Your Comment