9 Mei 2025 - 23:44
Source: Parstoday
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Muqawama utaendelea hadi ushindi kamili

Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema Muqawama utaendelea hadi ushindi kamili utakapopatikana na kuangamizwa kikamilifu utawala ghasibu na vamizi wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Naim Qassem ameasema hayo katika ujumbe wake wa video aliotoa kwa mkutano uliopewa jina la "Qom, Chuo cha Kidini, Mapinduzi ya Kiislamu na Muqawama," uliofanyika katika Chuo cha Dar al-Shafa - chuo mashuhuri cha wanafunzi wa kidini wa ngazi ya juu kilichoko katika mji wa Qom hapa nchini Iran.

"Tuna imani kamili na ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi, na Muqawama utaendelea hadi ushindi kamili na kuangamizwa kikamilifu wavamizi. Hakuna nguvu duniani inayoweza kuzuia matakwa ya Umma wa Kiislamu" amesisitiza Katibu Mkuu wa Hizbullah.

Aidha, Sheikh Qassem amesifu juhudi za wanazuoni wenye umaizi na uelewa katika Chuo Kikuu cha kidini cha Qom, ambacho, amekielezea kuwa ni "ngome dhidi ya dhulma na utaghuti," na kitovu cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo ndiyo yaliyohamasisha na kuleta mwamko wa harakati za ukombozi katika eneo zima.

Akikumbusha uvamizi uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi za Lebanon miongo kadhaa iliyopita, Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, Mapinduzi ya Kiislamu na fikra za kiongozi wake Imam Khomeini, ziliongoza mapambano ya taifa la Lebanon dhidi ya Wazayuni maghasibu.

"Baada ya ardhi yetu kuvamiwa, Mapinduzi ya Kiislamu na mawazo ya Imam Khomeini yakawa mwanga wetu wa kuongoza kwenye njia ya mapambano. Watu wa Lebanon, hususan wapiganaji wa Hizbullah, walianza kufuata njia ya Muqawama kwa kufuata uongozi wa Imam Khomeini," ameeleza Sheikh Qassem.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha