Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maja'lisi za Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (as) na Mashahidi wa Karbala zinaendelea katika Hawza ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-Salaam - Tanzania. Leo hii (Jana) tarehe 29 - 06- 2025, kwa mara nyingine Majlisi adhimu ya maombolezo ya Imam Hussein (as) ilifanyika katika Madrasa hiyo iliyosimamiwa na wanafunzi wenyewe mabinti wa Kiislamu wanaosoma katika Madrasa hii.
Walifungua Majlisi hiyo kwa Kisomo cha Qur'an Tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi hao anayeitwa: Mwanaidi Sultan. Kisha ikasomwa Ziarat Ashura kupitia Aidat Abdullah, ambaye pia ni Mwanafunzi wa Madrasat hii. Khutba katika mnasaba wa Maombolezo ya Muharram ilitolewa pia na Mwanafunzi, anayeitwa: Fatima Mauga.
Khatiba wa Majlis hii, (Fatima Mauga) alizungumzia mada muhimu iliyoitwa: "Masomo tunayojifunza kutoka Karbala". Katika mada hiyo, alijikita zaidi katika kufafanua na kudadavua nukta muhimu inayomhusu Mwanamke wa Kiislamu, ambayo aliipatia anuani isemayo: "Tunajifunza nini sisi kama Wanawake wa Kiislamu kutokana na yale maarifa tuliyojifunza, na upi wajibu wetu kwa wakati huu wa sasa?".
Mwisho: Kama tulivyodokeza hapo juu, Majlis hii imeandaliwa na kufanyika kupitia: Wanafunzi - Mabanati wa Madrasat ya Hazrat Zainab (sa) - iliyopo Kigamboni - Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.
Your Comment