Kwa mujibu wa taarifa, zaidi ya wanazuoni na wasomi 100 kutoka ulimwengu wa Kiislamu wametoa tamko maalum wakirejea upya msimamo wao wa kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, huku wakimtaja rais wa Marekani na waziri mkuu wa Israel kuwa ni muharib yaani adui wa Mwenyezi Mungu.
Kwa mujibu wa ofisi ya mahusiano ya umma ya Jukwaa la Umoja na Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu Duniani, tamko hilo, lililotolewa kwa lugha ya Kiarabu, Kiingereza na Kiajemi, liliangazia hoja kadhaa kwa mujibu wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu, Sunnah ya Mtume Muhammad (SAW), kanuni za Fiqhi ya Kiislamu na misingi ya sheria za kimataifa.
Tamko hilo lililaani vitisho vinavyotolewa na Marekani na Israel dhidi ya Iran na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na likasema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa utawala wa Israel Benjamin Netanyahu ni muharib kwa mujibu wa Aya ya 33 ya Surah Al-Ma’idah.
Wanazuoni hao pia walikemea vitisho vya Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, wakisema kuwa kutoa vitisho na kuweka masharti kwa mataifa ni mfano wa wazi wa uonevu na hakuna uhalali wowote wa kisheria wala wa kiakili.
Tamko hilo pia lilimtaja Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kuwa ni kiongozi wa safu ya heshima ya Kiislamu, na likasisitiza kuwa tishio lolote dhidi ya kiongozi huyo anayetukuzwa linachukuliwa kuwa uadui dhidi ya safu hiyo ya heshima ya Kiislamu.”
Wanazuoni hao wameitaka jamii ya Kiislamu, mataifa, vyombo vya habari, wanazuoni na wasomi, kuchukua msimamo ulio wazi, wa pamoja na wenye uwajibikaji katika kuunga mkono taifa la Iran na safu ya heshima ya Kiislamu.
Wamesisitiza kuwa:“Vitisho vya Trump dhidi ya Iran vilikuja baada ya waandamanaji wenye mwelekeo wa kifalme kufanya uharibifu wa mali za umma na binafsi katika miji kadhaa nchini Iran wiki iliyopita, na kusababisha vifo vya raia kadhaa pamoja na maafisa wa usalama, huku wengine wakijeruhiwa.”
Habari inayohusiana:
Ayatullah Khamenei: Iran haitalegeza msimamo na itakabiliana na magenge ya wahalifu
Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Iran walijitokeza tarehe 12 Januari kulaani ghasia na vitendo vya kigaidi, wakithibitisha upya utiifu wao kwa Mapinduzi ya Kiislamu na kulaani wale wanaohusika na kuvuruga utulivu wa taifa.”
“Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amewapongeza wananchi wa Iran kwa maandamano hayo makubwa na siku ya kihistoria waliyoiunda tarehe 12 Januari.”
Maandamano ya amani yaliyoanza mwishoni mwa mwezi Disemba, 2025 ya kulalamikia ugumu wa kufanya biashara na kushuka thamani sarafu ya taifa, yaliendelea kwa siku kadhaa kwa amani lakini uchochezi wa madola ya kibeberu uligeuza maandamano hayo kuwa ya ghasia, ukatili, vurugu, mauaji na uharibifu mkubwa wa mali za umma na za watu binafsi.
Your Comment