Sayyid Abbas Araghchi aliandika kwenye mtandao wa X: "Marekani imewekwa rangi ya manjano katika upande wa Magharibi wa dunia. Bahari kadhaa mbali, upande mwingine wa dunia, mipaka ya Iran pia imewekwa rangi ya manjano. Duara dogo jekundu linaonyesha Mlango-bahari wa Hormuz.
Jeshi la Marekani linalofanya kazi kwenye fukwe zetu, sasa linataka kutupangia jinsi majeshi yetu yenye nguvu yanavyopaswa kufanya mazoezi ya kijeshi katika ardhi yetu! CENTCOM inataka 'utaalamu' kutoka kwa jeshi la taifa ambalo serikali ya Marekani imeliita 'shirika la kigaidi', na wakati huo huo inatambua haki ya shirika hilo hilo kufanya mazoezi ya kijeshi!
Kiwango hiki cha utata ni ukweli ambao ulimwengu wa leo unakabiliana nao, na inashangaza kwamba serikali za Ulaya nazo zimeamua kufuata njia hiyo hiyo. IRGC imekuwa na inaendelea kuwa mlinzi wa amani na utulivu katika Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz. Katika kanda yetu, IRGC inatambulika vyema kama jeshi lenye nguvu lililothibitisha uwezo wake dhidi ya magaidi na wavamizi. Uhuru wa safari za baharini ni muhimu kwa Iran kama ulivyo kwa majirani zetu, lakini uwepo wa majeshi ya kigeni daima huleta mvutano badala ya usalama."
Your Comment