14 Februari 2026 - 13:09
Source: ABNA
Kukosoa kwa Hezbollah kwa Serikali ya Lebanon Kukaa Kimya Mbele ya Ukiukwaji wa Mamlaka ya Nchi Hiyo

Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hezbollah la Lebanon alisema hakuna juhudi zozote kubwa zinazoonekana za kumlazimisha adui kutekeleza ahadi za kusitisha mapigano.

Sheikh "Ali Damoush", Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hezbollah la Lebanon, alisisitiza kuwa upinzani haukuwa kamwe kitu kingine isipokuwa sababu ya nguvu na uthabiti kwa Lebanon; ni kanuni za upinzani ndizo zilizotuhifadhibia nchi na kwa kipindi cha miaka thelathini iliyoputa zimetoa ulinzi wa Lebanon na kuzuia utawala wa Kizayuni.

Katika khutuba yake ya Ijumaa aliyoitoa katika eneo la Hazrat Zainab (amani iwe juu yake) katika kitongoji cha kusini cha Beirut, alisema: "Serikali haikutimiza matarajio ya watu wa Lebanon na haikuweza kutekeleza majukumu yake na kuchukua wajibu wake - iwe kwa kukosa uwezo au kupuuza. Leo watu wanauliza serikali iko wapi? Kwa sababu watu wetu wameiona serikali katika misimamo tu ambayo haionyeshi matamanio na madai ya Walebanon; huku adui akikiuka mamlaka ya nchi, akiendelea na mauaji, mashambulizi ya mabomu na uharibifu, akikalia maeneo kwa mabavu, akiwazuia watu kurudi kwenye miji na vijiji vyao, na kujaribu kulazimisha eneo la kizuizini kwenye mipaka, lakini hakuna juhudi zozote kubwa zinazoonekana za kumlazimisha adui kutekeleza ahadi za makubaliano ya kusitisha mapigano".

Damoush alifafanua: "Serikali kama hiyo haiwajengei watu imani na si kimbilio kwao. Kila mtu anapaswa kujua kuwa watu wetu hawatasalimu amri na hawatarudi nyuma na wataendelea kusisitiza juu ya kuzingatia kikamilifu haki zao".

Alithibitisha tena kwamba upinzani ni haki halali na utaendelea kuwa ishara ya utu na heshima ya Lebanon, na hakuna mtu, awe wa daraja gani, anayeweza kuuondoa upinzani huu na haki yake ya kuwepo na kujilinda, au kufuta kutoka kwenye historia ya nchi dhabihu za wapiganaji na mafanikio yao katika suala la kukomboa na kulinda Lebanon.

Your Comment

You are replying to: .
captcha