Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Abna, utawala wa Kizayuni ndani ya masaa machache iliyopita umezidisha mashambulizi yake dhidi ya maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza ikiwemo kambi ya Nusayrat, Deir al-Balah na jiji la Gaza, ambapo katika mashambulizi haya angalau watu 8 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Katika jiji la Khan Yunis, utawala wa Kizayuni ulilishambulia kituo cha polisi kwenye makutano ya al-Masalh kwa ndege isiyo na rubani, shambulizi ambalo lilisababisha vifo vya watu 4.
Mashuhuda pia waliripoti kuwepo kwa watu wengine kadhaa waliojeruhiwa kwa hali mbaya kutokana na shambulizi hili.
Katika jiji la Gaza, watu wawili waliuawa kwa kupigwa na ndege isiyo na rubani.
Kuzidisha kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza kunatokea wakati hali ya kibinadamu katika ukanda huu ikiwa tete.
Your Comment