Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Gazeti la Israel Hayom limeripoti ongezeko linalotia wasiwasi la watu wa Israeli kuhusiana na kushirikiana kimaslahi na Iran, na limesema kuwa Shabak (Mamlaka ya Usalama wa ndani ya Israel) linafuatilia mwelekeo huu kwa tahadhari na wasiwasi mkubwa. Kulingana na ripoti hii, katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la kujaribiwa kuwashawishi watu, hasa ndani ya jamii ya Wayahudi wa Orthodox (Haredi), na angalau watu watano kutoka jamii hii tayari wamekamatwa wakihusishwa na ujasusi kwa ajili ya Iran.
Chanzo cha kiusalama kimeeleza kwamba mchakato huu kawaida huanza kwa misheni inayojionyesha kuwa rahisi, kama vile kupiga picha za mitaa au kusakinisha mabango, lakini baadaye unaweza kupelekea kuwapeleka kwenye misheni ya kiusalama yenye hatari na yenye siri kubwa.
Your Comment