27 Februari 2026 - 18:25
“Kinamasi cha Ghuba ya Uajemi”; Ujumbe wa Onyo wa Tehran kwa Washington | Tishio la Ayatollah Khamenei si la Mzaha

Kauli za Hani al-Jamal zinaonyesha kuwa misimamo ya Ali Khamenei inachukuliwa kwa uzito, huku akidai kuwa uwezo wa makombora na droni wa Iran pamoja na mbinu za vita visivyo vya moja kwa moja unaweza kubadili mizani ya nguvu katika eneo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Hani al-Jamal, akirejelea misimamo ya hivi karibuni ya Ali Khamenei, amesisitiza kuwa tishio la Iran dhidi ya Marekani ni la kweli na la kuchukuliwa kwa uzito. Amesema Tehran inaweza kutumia uwezo wake wa makombora na ndege zisizo na rubani (drones) kuharibu au kulemaza mifumo ya adui.

Ameongeza kuwa ubora wa Iran katika vita vya aina ya “asymmetrical warfare” unaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa mizani ya nguvu katika eneo la Ghuba na Mashariki ya Kati.

Your Comment

You are replying to: .
captcha