-
Hafla ya Ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya Jijini Arusha - Tanzania, kwa jina la Imam Ridha (a.s)
Wasomaji wa Kitaifa na Kimataifa wa Qur'an Tukufu wa Tanzania pamoja na Masheikh waliotoka maeneo mbalimbali ya nchi, ni miongoni mwa waliodhuhuria katika Hafla hiyo adhimu.
-
Ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya - Jijini Arusha, Tanzania
Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Leo hii (jana 17/3/2025) kumefanyika tukio muhimu kwa wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha, nalo ni ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya kwa jina la Imamu Ridha (a.s), chini ya Usimamizi wa Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa (a.s), inayoongozwa na Samahat Sheikh Maulid Hussein Kundya.
-
Swali kuhusu kadhia ya Palestina:
Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!
Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge: "Uislamu usiokuwa wa Ahlulbayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), huo umetengenezwa na Mayahudi au kama haukutengenezwa na Mayahudi basi umeingizwa mikono kwa asilimia 99% na Mayahudi".