-
Maandalizi na uhamasishaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 2025 / 1446H - Hawzat Imam Ali (as) Tanga - Tanzania
Hawzat Imam Ali (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga, Tanzania, Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Husein (a.s), Leo hii Jumatatu 21/04/2025, kimekutana na Waumini wa Bilal Muslim Bushiri na kuongea nao kuhusiana na Suala la Masira ya Imam Hussein (as) mwaka huu wa 1446H. Lengo la ziara hii, ni kuhamasishana zaidi na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Husen (a.s).
-
Viongozi wa JMAT ngazi ya Taifa Arusha-Tanzania, wakutana na Katibu Mkuu wa JMAT-TAIFA, Dr. Maasa Ole Gabriel na Naibu wake Sh.Dr. Abdur -Razak Amir
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Mh. Dr. Maasa Ole Gabriel, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa JMAT-TAIFA, Samahat Sheikh Dr. Abdur - Razak Amiri wamewakutanisha viongozi wote wa ngazi za juu waliopo katika Jiji la Arusha, ambapo wamekaa pamoja na kujadili masuala mbalimbali na muhimu katika Muktadha wa Maridhiano na Amani ya Taifa letu la Tanzania.
-
Mufti wa Burundi wa Madhehebu ya Ahlu-Sunna, Mh.Sheikh Ndikumagenge Masudi amtembelea Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari TIC Sheikh H. Jalala
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mufti Mkuu wa Burundi wa Madhehebu ya Ahlu-Sunna, Sheikh Ndikumagenge Masudi akiambatana na Mwenyekiti wake na watendaji wa Ofisi yake katika Ziara yake Nchini Tanzania, alipata fursa ya kumtembelea Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (T.I.C), Maulana Sheikh Hemed Jalala na kubadilishana fikra na mawazo katika suala muhimu la kuutumikia Uislamu na Waislamu.
-
Kikao maalum kati ya Mkuu wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Tanzania, Dr. Ali Taqavi na Mh.Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Kikao maalum kati ya Mkuu wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Tanzania, Dr. Ali Taqavi na Mh.Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi. Katika Kikao Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Dares-Salam - Tanzania amejadiliana na Mheshimiwa Mufti Mkuu wa Zanzibar kuhusiana upanuzi wa Chuo cha Qur'an Tukufu ndani ya Zanzibar, kuhudhuria kwa wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu wa Zanzibar katika Tamasha la Qur'an Tukufu, pamoja na maandalizi na upangaji ratiba muhimu kuhusiana na Tamasha hilo la Qur'an Tukufu litakalofanyika nchini Tanzania hivi karibuni. Katika Kikao hiki Dr. Ali Taqavi aliambatana pia na Sheikh Dr. Alhad Musa Salum, Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA.
-
Habari Pichani | Ziara ya Dr.Ali Taqavi katika Chuo cha Qur'an Tukufu cha Jamiat al-Mustafa (s) - Zanzibar - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hojjat al-Islam wal-Muslimin Dr.Ali Taqavi afanya Ziara muhimu katika Chuo cha Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania akiambata na Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA.
-
Habari Pichani | Sherehe ya Kipekee ya Kufikia Umri wa Dini (Taklif) kwa Wasichana wa Karbala
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Sherehe ya bulugh kwa wasichana imefanyika kwa adhama katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq. Takribani wasichana 5,000 kutoka shule 121 walishiriki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Ataba ya Abbasiyya. Tukio hilo lililenga kuwapa wasichana hawa utambuzi wa kidini na kuadhimisha hatua muhimu ya kuingia katika umri wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Sherehe hiyo imekuwa tukio lenye mvuto mkubwa, likiambatana na hotuba, mawaidha na maombi, na kuwapa washiriki fursa ya kuimarisha uhusiano wao na mafundisho ya AhlulBayt (a.s).
-
Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sheikh Ridha Dosa akitoa Somo la Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania, katika Chuo cha Qur'an Tukufu cha Jamiat Al- Mustafa (s) kinachoongozwa na kusimamiwa na Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Hojjat al-Islam wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi.
-
Ujue wajibu wako katika kuiongoza familia yako + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Samahat Sheikh Reihan Yasin, akifafanua mada Muhimu kuhusu mtu kuujua Wajibu wake katika kuiongoza familia yake.
-
Putin aidhinisha Makubaliano ya kina ya kimkakati na Iran
Mkataba huo unalenga kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika maeneo yote yenye maslahi ya pamoja.