-
Ziara ya Dkt. Ali Taqavi, Mkuu wa Jamiat Al-Mustafa(s) Tanzania, katika Shule ya Abul Fadhli Al-Abbas(as), Tanga Mjini
Mkurugenzi wa shule hiyo, Sheikh Shafi Nina, alieleza kufurahishwa kwake na ziara hiyo, akiitaja kuwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mahusiano na taasisi za kitaifa na kimataifa kwa ajili ya mafanikio ya Kisayansi kwa vijana wa Kitanzania.
-
Dkt. Ali Taqavi Afanya Ziara Muhimu katika Shule ya Mustafa, Tanga – Tanzania + Picha
Mazungumzo yalijikita katika masuala muhimu ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na njia bora za kuimarisha elimu, kuinua viwango vya ufaulu, na kueneza Sayansi za Ahlul-Bayt (as). Aidha, walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano na mshikamano baina ya taasisi za kielimu kwa lengo la kukuza maarifa ya Kiislamu na maadili mema kwa vijana.
-
Ziara ya Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam, Tanzania, Dr.Ali Taqavi katika Shule za Abu al-Fadhl al-Abbas, Mustafa na Qaem – Jijini Tanga
Lengo kuu la ziara hii lilikuwa ni kutathmini hali ya elimu katika shule hizo, na kujadili fursa za ushirikiano hasa katika eneo la kufundisha wa Elimu za Qur'an Tukufu na Sayansi za Kidini kwa ujumla.
-
Ziara ya Viongozi wa Kidini Katika Hawzat Al-Qaim (as), Tanga - Tanzania + Picha
Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), akiambatana na Dkt. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) nchini Tanzania, pamoja na Samahat Sayyid Arif Naqvi, walitembelea Hawzat Al-Qaim (as) iliyopo Tanga Mjini, Barabara ya 5.
-
Kikao Maalum na Mufti Mkuu wa Tanzania pamoja na Sheikh wa Mkoa wa Tanga + Picha
Kikao hiki kilikuwa na madhumuni ya kujadili maandalizi ya kuandaa hafla ya usomaji wa Qur’ani Tukufu katika uwanja wa michezo wa jiji la Tanga, na kililenga kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha tukio hilo linakuwa la mafanikio na lenye athari chanya kwa jamii ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla.