22 Mei 2023 - 05:11
Cameroon iliyogawanyika yaadhimisha Siku ya Umoja wa Kitaifa

Cameroon imeadhimisha miaka 51 kama taifa lenye umoja kwa kufanyika gwaride la kijeshi na kiraia katika Siku ya Umoja wa Kitaifa iliyoadhimishwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Yaounde. Rais Paul Biya amekuwepo madarakani huko Cameroon kwa muda wa miaka 41. Akiwa na umri wa miaka 91, Rais wa Cameroon ndiye mkuu wa nchi mweye umri mkubwa zaidi duniani.

Cameroon hivi sasa imegawanyika na  haina umoja kama ule uliokuwa ukishuhudiwa huko nyuma. Maelfu ya watu wameuawa tangu mwaka 2016 huku zaidi ya watu milioni moja wakilazimika kuyahama makazi yao baada ya kundi la Wacameroon wanaozungumza lugha ya Kiingereza kuanza kupigana dhidi ya serikali ya Rais Biya inayozungumza lugha ya Kifaransa.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wa Cameroon walioshiriki katika maadhimisho hayo na kushuhudia gwaride hilo lal kijeshi na kiraia katika Maadhimisho ya  Siku ya Umoja wa Kitaifa walionekana kuwa na matumaini kuhusu mustakabali wa nchi yao na kukaribisha siku hii.

 Therese Temgoua raia wa Cameroon mfanyakazi wa benki anayeishi katika eneo linalozungumza lugha ya Kifaransa nchini humo anasema:" Maadhimisho hayo yanawakumbusha kuwa wao ni wamoja, na kwamba wanaweza kuishi kwa pamoja kwa amani na furaha. Wakati huo huo Enobi Akepe raia wa Cameroon mhadhiri wa Chuo Kikuu anayezungumza lugha ya Kiingereza anasema: Nadhani siku hii ni siku ya furaha, kile nilichokiona kinadhihirisha kuwa demokrasia ya Cameroon iko katika mkondo sahihi.  

Inafaa kuashiria hapa kuwa ghasia na mapigano yaliripotiwa huko Cameroon  mwaka wa 2017, wakati kundi moja la wanamgambo lilipotangaza kuwa taifa huru katika mikoa ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-magharibi mwa Cameroon katika maeneo ya watu wachache wanaozungumza lugha ya kiingereza katika nchi inayozungumza Kifaransa.

342/