Kwa mujibu wa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, hafla ya kumkumbuka Mpigana Jihadi Katika Njia ya Allah, Sayyid Azizi wa Umma wa Kiislamu, Shahidi Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Hassan Nasrallah na wenzake akiwemo kamanda Shahidi Nilforushan, itahudhuriwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu siku ya Ijumaa, Oktoba 4, kuanzia saa nne asubuhi Tehran, katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (RA).
Katika hafla hiyo inayofanyika kufuatia kuuawa shahidi mshika bendera ya muqawama na uhuru wa Quds na Palestina, Seyyed Hassan Nasrallah, na katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa kwanza wa Operesheni ya Kimbunga cha Al- Aqsa ya wapiganaji wa harakati za muqawama (mapambano ya Kiislamu ya Palestina), Sala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran, Oktoba 4, itaswalishwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Ukumbi wa Swala wa Imam Khomeini (RA).
342/