12 Machi 2025 - 18:26
Source: Parstoday
Hamas yasema hatua ya Israel kuzuia misaada kuingia Gaza ni ‘Uhalifu wa Kivita’

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imesema kuwa uamuzi wa utawala haramu wa Israel wa kuzuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu na mahitaji ya msingi katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa ni "uhalifu wa kivita."

Katika taarifa, Hamas imesema kuwa kufungwa kwa mipaka kunakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya Januari. Hamas imesema: "Hatua hii ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu, Mikataba ya Geneva, na inachukuliwa kama uhalifu wa kivita na adhabu ya pamoja inayotishia maisha ya raia wasio na hatia."

Hamas imesema kuwa kufungwa kwa mipaka na kuendelea kuzuiwa kwa misaada kwa siku ya 10 mfululizo "kunazidisha mateso ya zaidi ya Wapalestina milioni mbili" na "kunatishia njaa kubwa" huko Gaza.

"Kuzuia chakula, dawa, mafuta, na misaada ya msingi kumesababisha kupanda kwa bei ya chakula na upungufu mkubwa wa vifaa vya matibabu, hali inayozidisha mgogoro wa kibinadamu huko Gaza."

Taarifa hiyo pia imesema kuwa "kuzuia kuingia kwa mashine nzito kunatatiza juhudi za kuondoa miili iliyozikwa chini ya vifusi, pamoja na juhudi za ukarabati na ujenzi wa upya wa Gaza."

Hamas imetoa wito kwa wasuluhishi kuishinikiza Israel kutekeleza ahadi zake chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano. Utawala haramu wa Israel ulianzisha kampeni ya mauaji ya kimbari huko Gaza tarehe 7 Oktoba 2023. Kufikia sasa, zaidi ya Wapalestina 48,500 wameuawa katika eneo hilo, wengi wakiwa ni wanawake na Watoto.

Mwezi Januari, utawala haramu wa Israel ulilazimika kuafiki mapatano ya kusitisha mapigano na Hamas baada ya kushindwa kufanikisha malengo yake.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha