Ayatollah Makarim Shirazi amethibitisha kwamba Baraza la Uratibu wa Matangazo ya Kiislamu lina mchango mkubwa usio na mfano katika kuhifadhi mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Ni wajibu kwa Waislamu kote duniani kuwafanya maadui hawa wajute kwa matamshi na vitendo vyao. Na ikiwa Waislamu watapata mashaka au hasara kutokana na kusimama dhidi yao, basi wao watakuwa na thawabu ya mujahid (mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu), Insha'Allah.
Ayatollah Makarem Shirazi, Miongoni mwa Marjii Taqlid, amewaalika Waislamu ili kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alifafanua akisema: Ni muhimu kwa viongozi na marais wa nchi za Kiislamu kuazimia na kuhakikisha azma yao ya kuacha kutojali na kupuuzia jinai za Wazayuni.