27 Machi 2025 - 02:24
Maandamano ya Siku ya Quds ni Nguvu ya Moyo kwa Mujahidina na Wanyonge wa Palestina na Lebanon

Ayatollah Makarem Shirazi, Miongoni mwa Marjii Taqlid, amewaalika Waislamu ili kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alifafanua akisema: Ni muhimu kwa viongozi na marais wa nchi za Kiislamu kuazimia na kuhakikisha azma yao ya kuacha kutojali na kupuuzia jinai za Wazayuni.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Hazrat Ayatollah Makarem Shirazi, amewaalika na kuwahimiza Waislamu kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds, ambapo amesema: Ni muhimu kwa Viongozi na Marais wa nchi za Kiislamu kuwa imara katika azma yao na kutopuuzia jinai za Wazayuni.

Soma ujumbe wa kina wa Ayatollah Makarem Shirazi katika Mnasaba wa Siku ya Quds Duniani hapa chini kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Kila mwaka, Ijumaa ya Mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Siku ya Mshikamano wa Waislamu wote na watu huru wa dunia nzima katika kutetea Haki halali za Wananchi Madhulumu wa Palestina, na kuunga mkono kukombolewa kwa Msikiti wa Al-Aqsa kutoka kwa wanyakuzi wake (Mazayuni).

Katika mwaka uliopita, matukio ya kuhuzunisha ya mashambulizi ya kinyama ya utawala haram wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na Miji na vijiji vingine vya Palestina na Lebanon yalishuhudiwa na watu wote wa dunia. Wanawake, Watoto, na Wazee walilengwa na mabomu ya tani nyingi katika nyumba zao, wagonjwa walichomwa moto wakiwa hai Hospitalini, na vijana waliuawa kwa kupigwa risasi moja kwa moja. Utawala huu wa umwagaji damu, kwa sapoti na uungaji mkono wa Marekani, haukuacha jinai yoyote dhidi ya watu wasio na hatia, na Serikali za Magharibi, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi zinazodai Haki za Binadamu hazikuchukua hatua zozote za dhati kuzuia jinai hizo.

(Insha Allah) Mwenyezi Mungu akipenda, Waislamu wote Duniani watakuwa ni chemchemi ya faraja na nguvu kwa Mujahidina na wale wadhulumiwa huko Palestina na Lebanon kwa kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, sambamba na kulaani jinai za utawala huo haram bandia.

Vile vile ni lazima kwa viongozi wa nchi za Kiislamu kudhamiria na kuimarisha azma zao na kutumia njia yoyote iwezekanayo kuwasaidia Wananchi wanaodhulumiwa na kutopuuzia jinai hizo.

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie heshima, izza ya Uislamu na Waislamu na kuwaangamiza maadui wa Uislamu hususan utawala haram na ghasibu wa Kizayuni.

وَسَیعلَمُ الّذینَ ظَلَموا أَی مَنقَلَبٍ ینقَلِبونَ

"Na watajua Madhalimu ni mgeuko upi wanaogeuka".

Qom - Nasser Makarem Shirazi
Tarehe 25 Ramadhani, 1446 A.H

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha