Ayatollah Mojtaba Khamenei
-
Kiongozi wa Iran: Ukiukaji wa Marekani unathibitisha saini yake haina thamani; Iran ina masomo yasiyosahaulika kwa adui
Katika ujumbe kuhusu kuaga kwa kishujaa kwa Kiongozi shahidi wa Iran, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Mojtaba Khameni amesema kuwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Marekani wa makubaliano yaliyosainiwa kati ya marais wa Iran na Marekani umeonyesha tena kuwa saini ya rais wa Marekani haina thamani. Amesema pia kuwa Iran na mhimili wa muqawama wana masomo yasiyosahaulika kwa adui, kama ilivyoonekana kupitia ujasiri wa wapiganaji na uhodari wa wananchi wa maeneo ya kusini.
-
Mazingira ya Mazishi ya Imam Shahidi (r.a) Kufanyika kwa Maelekezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya Kuaga na Kusimamia Mazishi ya Imam Shahidi (r.a) amesema kuwa maandalizi ya mazishi hayo yanafanyika kwa uongozi na maelekezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, huku akizitaka vyombo vya habari kuhifadhi tukio hilo la kihistoria kwa ajili ya vizazi vijavyo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi Atoa Ujumbe kwa Wairan Kuhusu Makubaliano kati ya Iran na Marekani
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema aliruhusu kutiwa saini kwa hati ya makubaliano kati ya Iran na Marekani baada ya kupokea dhamana kutoka kwa Rais wa Iran kwamba haki za wananchi wa Iran na Kambi ya Muqawama zitalindwa, huku akisisitiza kuwa mazungumzo ya baadaye hayatamaanisha kujisalimisha kwa matakwa ya Marekani.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kumtambua Imam Khomeini ni Taa ya Kuongoza Mustakabali wa Iran
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, amesema kuwa kuelewa na kumtambua Ruhollah Khomeini ni mwanga unaoongoza mustakabali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amebainisha kuwa kufuata mwenendo wa Ali ibn Abi Talib kumekuwa alama ya fahari kwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku akisisitiza kwamba taifa la Iran limesimama bega kwa bega na Muqawama na kuwa mfano wa kujivunia kwa mataifa yanayotafuta uhuru. Aidha, amewataka wananchi kudumisha umoja, busara na kuaminiana ili kuvuruga njama za maadui na kulinda mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Ayatollah Mojtaba Khamenei Aonya Dhidi ya Njama za Kusababisha Mgawanyiko wa Kijamii Iran
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza umuhimu wa kulinda umoja wa wananchi, akionya kuwa adui anatumia mbinu za kueneza mifarakano ya kijamii baada ya kushindwa kufikia malengo yake kupitia mashinikizo ya kijeshi, kiuchumi na kisiasa.