Bakwata
-
Mufti Mkuu Sheikh Dkt. Abubakar Zubair akutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa na kujadili kuhusu njia za Kuimarisha Maadili na Ucha Mungu katika Jamii
Ziara hii ya Mufti Mkuu ni miongoni mwa juhudi endelevu za uongozi wa Kiislamu nchini katika kujenga maadili, amani na mshikamano wa kijamii, sambamba na kutoa wito wa kuzingatia uadilifu na uchamungu katika kila nyanja ya maisha.
-
Sheikh Hemed Jalala na Sheikh wa Mkoa wa Tabora (BAKWATA) waonyesha: Matendo ya Hekima Yanayounganisha Watu na Kuimarisha Umoja wa Kiislamu
Kwa hakika, ziara hii ni kielelezo cha Uislamu wa kweli uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) - Uislamu wa upendo, udugu, na umoja. Kama alivyonena Imam Ali (a.s.): "Kuweni walinganizi wa watu bila kutumia maneno yenu, bali kwa matendo yenu.” (Nahjul-Balagha, Hikma 31)
-
Maulana Sheikh Hemed Jalala Aendelea kuimarisha Umoja wa Waislamu Kupitia Ziara ya Kidini Nchini Tanzania
Katika moja ya sehemu za ziara yake, Maulana Sheikh Hemed Jalala alitembelea Mkoa wa Kigoma, ambapo alipokelewa kwa mapokezi mazuri kutoka kwa waumini na viongozi wa dini wa eneo hilo. Moja ya matukio muhimu katika ziara hiyo ni kukutana kwake na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma (BAKWATA), Samahat Sheikh Hassan Kiburwa, katika ofisi za BAKWATA Mkoa wa Kigoma, ambapo viongozi hao wawili walifanya mazungumzo ya kina kuhusu maendeleo ya Uislamu, umoja wa Waislamu, na namna bora ya kuimarisha harakati za kidini nchini.
-
BAKWATA Manyara wafanya Kikao cha Halmashauri Bakwata Mkoa Jumapili
Kikao hiki ni Kikao cha Kawaida cha Kikatiba cha Halmashauri ya Mkoa.
-
Dar es Salaam, Tanzania - Mei 2025:
BAKWATA Yatangaza Rasmi Tarehe ya Sikukuu ya Eid El-Adh’ha: Jumamosi, Juni 7, 2025
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, Alhaj Nuhu Jabiri Mruma, ambapo imeelezwa kuwa sherehe za kitaifa za Eid El-Adh’ha mwaka huu zitafanyika jijini Dar es Salaam, katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Makao Makuu ya BAKWATA – Kinondoni.