15 Julai 2025 - 13:23
BAKWATA Manyara wafanya Kikao cha Halmashauri Bakwata Mkoa Jumapili

Kikao hiki ni Kikao cha Kawaida cha Kikatiba cha Halmashauri ya Mkoa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Uongozi wa Halmashauri Bakwata Mkoa wa Manyara umefanya kikao cha kawaida cha kikatiba cha Halmashauri ya Mkoa.

Taarifa ya katibu wa BAKWATA Mkoa huo Alhaj Ahmadi Khayrallah amesema hicho ni kikao cha kikatiba anbacho hufanyika kila baada ya miezi sita.

Amesema miongoni mwa agenda ilikuwa ni kupanga kufanyika kwa mkutano mkuu wa kawaida wa kila Mwaka, kuweka mipango ya maendeleo, kuanzisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vyanzo vilivyopo.

Kufanya vikao vya Taasisi ni ndiyo nguzo kuu ya afya taasisi hiyo na pongezi kwa Bakwata Manyara kwa desturi ya kufanya vikao vyote vya kikatiba na kuhakikisha vikao hivyo vunaibua mipango na mikakati mizuri na mikubwa kwa maendelea ya Waislam wa mkoa wa Manyara na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Bakwata Mkoa wa Manyara ambayo hivi karibuni imefanyiwa ukarabati mkubwa na baada ya kikao wajunbe walitembelea kukagua mirai mbalimbali ya BAKWATA mjini Babati.
Habari hii ni kwa hisani kubwa ya:

Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Jumanne 15.7.2025.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha