Mchambuzi wa zamani wa CIA Larry Johnson amesema mashambulizi dhidi ya Iran wakati mazungumzo yakiendelea yanaashiria juhudi za kuhujumu mchakato wa kidiplomasia, akionya kuwa huenda eneo hilo likashuhudia duru mpya ya mvutano katika siku zijazo.
Johnson anaamini kuwa Iran sasa si tu haiko dhaifu, bali imejizatiti kama mchezaji mkuu katika masuala ya kieneo, na ina uwezo wa kushughulikia changamoto na shinikizo kutoka nje.