-
Jarida la Foreign Affairs: "Uwezo wa Marekani Hautoshi Tena Kutimiza Malengo Yake ya Kimataifa"
Uchambuzi wa jarida la Foreign Affairs unasema kuwa kuongezeka kwa vitisho katika Mlango wa Hormuz na maendeleo ya teknolojia za kijeshi kumeonyesha pengo kati ya matarajio ya kimataifa ya Marekani na uwezo wake halisi wa kudhibiti usalama wa bahari duniani.
-
Iran: Mashambulizi ya Marekani Dhidi ya Meli za Kibiashara Ni Tishio kwa Usafiri wa Baharini wa Kimataifa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amesema mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Marekani dhidi ya meli za kibiashara za India yanatishia usalama wa usafiri wa baharini wa kimataifa na kuyataja kuwa ni mfano wa uharamia wa baharini.
-
Gharibabadi: Umoja wa Ardhi na Usalama wa Taifa la Iran Si Sehemu ya Propaganda za Kisiasa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema Iran haitaruhusu mamlaka yake, umoja wa ardhi wala usalama wa taifa kuwa sehemu ya propaganda au mashinikizo ya kisiasa kutoka kwa Marekani na washirika wake.
-
Rais Pezeshkian: Umoja wa Kitaifa Ndiyo Mtaji Mkubwa Zaidi wa Iran Katika Kipindi Hiki
Rais Masoud Pezeshkian amesema mshikamano wa kitaifa ndio msingi wa maendeleo ya Iran, akisisitiza matumizi ya uwezo wa wataalamu na kujibu mahitaji ya wananchi ili kutatua changamoto zinazoikabili nchi.
-
Khatibu wa Ijumaa Tehran Aonya Marekani na Israel: Mkivuka Mipaka Mtajibiwa kwa Nguvu
Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema Rais Donald Trump na Benjamin Netanyahu watakabiliwa na jibu kali na la uthabiti iwapo wataendelea na uchokozi dhidi ya Iran.
-
IRGC: Marekani Itajutia Ikiamua Kurudia Makosa Yake ya Zamani
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Hussein Mohabbi, amesema Marekani itajutia endapo itajaribu kurudia kile alichokiita majaribio yake yaliyoshindwa dhidi ya Iran.
-
Nyumba Rahisi Aliyoishi Kiongozi Mkuu wa Iran Yazua Hisia Mitandaoni +Video
Picha mjongeo ya nyumba aliyokuwa akiishi Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, imesambaa mitandaoni ikielezewa kuwa ni mfano wa maisha ya unyenyekevu na kujitolea kwa ajili ya Uislamu na Akhera.Nyumba hii inapatikana katika Mji wa Mash-Hadi, na ameishia ndani ya nyumba hiyo kwa muda wa miaka 55.
-
Chanzo Chafichua Rasimu ya Vipengele 14 vya Makubaliano Yanayodaiwa Kupendekezwa kati ya Iran na Marekani
Chanzo kilicho karibu na timu ya mazungumzo ya Iran kimefichua rasimu ya makubaliano yenye vipengele 14 vinavyohusisha usitishaji wa uhasama, kuondolewa kwa vikwazo, kufunguliwa kwa Mlango wa Hormuz, pamoja na kuachiliwa kwa mabilioni ya dola za mali za Iran zilizogandishwa.