Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Hussein Mohabbi, ameonya kuwa Marekani itajutia iwapo itaamua kurudia kile alichokiita majaribio yake yaliyoshindwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza katika taarifa yake, Brigedia Jenerali Mohabbi alinukuu methali maarufu inayosema: "Anayerudia jambo ambalo tayari limeshajaribiwa na kushindwa, mwisho wake ni majuto."
Alisema kuwa yeyote anayelazimisha kurudia majaribio yaliyofeli hapo awali hatavuna chochote isipokuwa majuto.
"Marekani ikiwa inataka kurudia tena kushindwa kwake kwa mara nyingine, basi bila shaka itajikuta ikijutia uamuzi huo," alisema msemaji huyo wa IRGC.
Kauli hiyo imekuja wakati mvutano kati ya Iran na Marekani ukiendelea kushuhudia misuguano ya kisiasa na kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Your Comment