Hii ni miaka 1187 tangu Imam Mahdi (AF) aingie katika kipindi cha Ghaiba Kubwa. Tukio hili ni fursa ya kuhuisha upendo wetu kwake, na kuonyesha kuwa taifa la Iran, hasa Qom, linasimama imara katika njia ya Imam wa Zama."
Shughuli za Imam Hadi (a.s) zilikuwa na nafasi muhimu katika kuhifadhi utambulisho wa kiakili na imani wa Waislamu wafuasi wa Madhehebu ya Shi'a Ithna Ashari. Uongozi wake wa kiroho na wa fikra kwa Shi'a waliokuwa Samarra, kuimarisha mtandao wa mawasiliano kati ya wafuasi wa Ahlul Bayt(as), na kusimama imara dhidi ya shinikizo la wa Abbasi, ni miongoni mwa huduma muhimu za Imamu Hadi katika maandalizi ya Shi'a kwa zama za Ghaibat Kubwa (Kutoonekana kwa Muda Mrefu).