Financial Times imekosoa vikali mbinu za Jared Kushner na Steve Witkoff katika diplomasia ya Marekani, ikisema mtazamo wao wa kibiashara na ukosefu wa uzoefu wa jadi wa kidiplomasia umechangia kushindwa kupata mafanikio katika migogoro ya Ukraine, Gaza na Iran.
Iran na Pakistan zasisitiza kuimarisha mabadilishano ya kibiashara na kiuchumi, hususan katika sekta ya nishati, kwa kuzingatia uwezo na maeneo ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amezungumza kwa njia ya simu na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya kikanda na kimataifa, huku akilaani vikali shambulio la kijeshi la Ukraine dhidi ya meli ya kibiashara ya Iran katika Bahari ya Caspian.