Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amesema mashambulizi ya kujihami ya Iran yalilenga malengo ya kijeshi pekee, akisema ripoti rasmi ya Qatar iliyowasilishwa kwa Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) imethibitisha hilo.
Mwanachama wa Baraza la Kutambua Maslahi ya Taifa la Iran, Jenerali Mohsen Rezaei, amesema Rais wa Marekani Donald Trump amekubali kuachia dola bilioni 24 za mali za Iran zilizokuwa zimezuiwa, ingawa hataki kutangaza uamuzi huo hadharani.
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wa Mkoa Mkuu wa Tehran amesema:
“Katika vita vya kujihami vya siku 12, tulisimama dhidi ya Marekani, utawala wa Kizayuni na jumla ya majeshi ya NATO. Kwa hakika, tuliwashinda wote wa NATO, jambo ambalo halijawahi kutokea.”