Licha
-
Gharib Abadi: Nguvu za Kijeshi za Iran Zililazimisha Adui Kuketi Mezani; Hati ya Mwisho ya Makubaliano Yakamilika
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Gharib Abadi, amesema nguvu za kijeshi za Iran ndizo zilizomlazimisha adui kurejea kwenye mazungumzo, akisisitiza kuwa maandishi ya mwisho ya hati ya maelewano yamekamilika na kutiwa saini rasmi kutafanyika Ijumaa nchini Uswisi, huku Iran ikiahidi kujibu hatua yoyote ya kutotekelezwa kwa ahadi za upande wa pili.
-
Hadhramaut; Moyo wa Mafuta wa Yemen na Kitovu cha Ushindani kati ya Saudi Arabia na Falme za Kiarabu (UAE)
Mkoa wa Hadhramaut, eneo kubwa zaidi na lenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Yemen, kwa sasa umegeuka kuwa kitovu cha ushindani kati ya Saudi Arabia na Falme za Kiarabu. Licha ya vita vilivyoendelea kwa zaidi ya muongo mmoja, Hadhramaut kwa kiasi kikubwa imeepuka mapigano ya moja kwa moja kati ya serikali ya Yemen iliyojiuzulu na serikali inayoungwa mkono na Harakati ya Ansarullah; hata hivyo, mkoa huu haujaepuka athari za vita na mashindano ya ushawishi wa ndani na kikanda.
-
Mwakilishi wa Ayatullah Sistani:
Licha ya juhudi zote, bado haki ya kueleza na kuonesha kikamilifu ukubwa wa Arbaeen haijatimizwa
Mwakilishi mwenye mamlaka kamili wa Ayatollah Sistani nchini Iran amesema kuwa Arbaeen ni fursa kubwa sana kwa wasimamizi na wenye dhamana wa tukio hili la kimataifa, na hawapaswi kupuuzia au kughafilika na thawabu na malipo makubwa yanayopatikana kutokana nalo.