Maarufu
-
Je, Taurati imebadilishwa? Angalia jibu la Qur’an hapa!
Kuhusu taarifa (maelezo) ya Qur’an Tukufu kuhusu ubadilishaji wa maneno ya Taurati, kuna mjadala wa kiitihadi kama ifuatavyo: 1. Mtazamo maarufu (ushahidi unaoonekana wazi kabisa katika Quran) Watafiti wengi na wafuasi wa mtazamo huu wanaona kwamba Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maneno kwa uwazi jabisa. Qur’an inataja maneno yaliyopinduliwa au kuharibiwa na baadhi ya Watu wa Kitabu (Ahlul-kita'bi): «يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَوَاضِعِهِ» (An-Nisa 46) Hapa (kwa mujibu wa Aya hiyo Tukufu) , ubadilishaji huo unahusiana na maneno yenyewe, na si tafsiri tu. 2. Mtazamo wa wapinzani (Mukhalifuna) Wao wanasema kuwa Qur’an inazungumzia ubadilishaji wa maana, si maneno ya kifasihi: Wanasema kuwa maneno ya msingi hayajabadilishwa, lakini maana au tafsiri potofu ndizo zilizobadilishwa au kutumika vibaya. Hii inaitwa ubadilishaji wa maana (tafsiri) badala ya ubadilishaji wa maneno.
-
Mwigizaji wa Australia Aukosoa Vikali Utawala wa Kizayuni kwa Kutojali Maisha ya Wapalestina
Amesema: “kila siku nashuhudia dharau na kutojali maisha ya Wapalestina kwa upande wa Waisraeli,” akieleza kuwa mwenendo huo ni “wa aibu” na kwamba wale wanaotekeleza “matendo haya mabaya” wanairudisha nyuma ubinadamu kila siku.
-
Taarifa za Hivi Punde:
Kuhusu Kuachiwa kwa Wafungwa Maarufu wa Kipalestina / Hatma ya Mwili wa Shahidi Yahya Sinwar Katika Mkataba wa Kusitisha Mapigano
Sambamba na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Harakati ya Mapambano ya Kipalestina (Muqawama) na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza, vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti tetesi na tafsiri tofauti kuhusu masharti ya makubaliano hayo na namna yatakavyotekelezwa.
-
Ibn Sirin ni Nani? - Mtazamo wa Kiislamu kuhusu Mtu Huyu na Sifa Zake
Abu Bakr Muhammad bin Sirin - Maarufu kama "Ibn Sirin" hakuwahi kuzungumza na mama yake kwa sauti ya juu, na kila alipomwambia jambo, ilikuwa kana kwamba anataka kulinong’oneza kwa siri.