Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum: "Wakenya ni ndugu wa Watanzania, na mbali na uhusiano wa kijamii, ni ndugu wa damu. Tunatambua kuwa mizozo hii inahusu zaidi vijana wa Kenya, lakini ni muhimu kuwakumbusha kuwa heshima ni nguzo muhimu katika mahusiano ya mataifa. Tunaamini Kenya ina Viongozi wa Dini na Serikali wanaoweza kusaidia katika hili."
Kuwatukana viongozi wakubwa wa kidini, daima imekuwa moja ya masuala nyeti na changamoto katika jamii za kidini. Jambo hili sio tu linaumiza hisia za waumini, lakini pia linaonyesha upungufu wa maadili na tabia mbaya ya wadhalilishaji.