Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (AS), Hojjat al-Islam Wal-Muslimin, Muhammad Hossein Amin, Mwandishi na Mtafiti wa masuala ya kidini, katika makala ya kipekee ya Abna, amechunguza matusi (na udhalilishaji) kwa Ahlul-Bayt (AS) na chimbuko na shakhsia ya wenye kuwakosea adabu.
Kuwatukana wakubwa wa kidini daima kumeleta athari kali na wakati mwingine vurugu katika ki[indi chote cha historia. Tabia hii inayofanywa na baadhi ya watu wenye malengo ya kisiasa, kiutamaduni au kidini, inatokana na udhaifu wa kiakili na utu wa watoa matusi (au wadhalilishaji) hao. Katika jamii za kidini, wakubwa wa kidini wanajulikana kama vielelezo vya maadili na kiroho, na kuwatukana (au kuwakosea adabu) kunachukuliwa kuwa ni matusi kwa maadili ya msingi ya jamii.
1. Nafasi ya wakubwa wa kidini katika Dini mbalimbali
1-1. Uislamu na watu watakatifu (Shakhsia Takatifu)
Katika Dini ya Kiislamu, heshima kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt (a.s) ni moja ya kanuni za kimsingi za imani. Aya za Qur'an Tukufu zinasisitiza kwa uwazi kabisa ulazima wa kumtukuza na kum,heshimu Mtume Muhammad (s.a.w.w):
«إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِکَتَهُ یُصَلُّونَ عَلَی النَّبِیِّ ۚ یَا أَیُّهَا الَّذِینَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَیْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِیمًا» (احزاب: ۵۶).
"Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu"(1)
Kumtukana (kumkosea adabu, kumvunjia heshima, na kumdhalilisha) Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) hakulaaniwi tu kwa mtazamo wa Sheria ya Kiislamu, bali katika historia yote, kumesababisha misimamo mikali kutoka kwa Waislamu.
Mfano wa wazi wa hili ulikuwa ni uchapishaji wa katuni za kuudhi dhidi ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) katika machapisho ya Magharibi, ambayo yalizua wimbi la maandamano ya kimataifa (2).
1-2. Kuheshimu wakubwa wa kidini katika Ukristo na Uyahudi
Katika Ukristo, Yesu (A.S) na Mariamu (S.A) wana nafasi muhimu na maalum. Kuwakosea adabu na kuwadhalilisha watu hawa katika jumuiya za Kikristo kunachukuliwa kuwa ni matusi kwa watakatifu hawa. Katika Uyahudi, watu kama vile Nabii Musa (A.S) na Nabii Daudi (A.S) wanaheshimiwa sana. Kuwatukana wakubwa hawa (katika dini hizo) kwa kawaida huhusishwa na radiamali na athari za kijamii na hata za kisheria (3).
2. Sababu za kuwatukana wakubwa wa kidini
1-2. Nia za Kisiasa
Matusi mengi (udhalilishaji mwingi) kwa wakubwa wa kidini hufanywa kwa lengo la kudhoofisha hadhi ya kidini na uhalali wa kiroho wa viongozi wa dini. Wakati wa zama za makhalifa wa Bani Umayyad na Bani Abbas, kuharibu sura (na heshima) ya Ahlul-Bayt (A.S) kulitumika kama chombo cha kudumisha nguvu zao za kisiasa (4).
2-2. Nia za Kitamaduni na Kijamii
Baadhi ya matusi husababishwa na ukosefu wa ufahamu wa kitamaduni na udhaifu katika kuelewa mafundisho ya dini. Katika jamii za kimagharibi, kukosekana kwa ufahamu sahihi wa nafasi ya Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt (a.s) kumewafanya watu kuwa wa wajinga wa kuyatukana kwa urahisi kabisa matukufu ya Uislamu(5).
2-3. Motisha za Kisaikolojia
Uchunguzi wa kisaikolojia unaonyesha kuwa tabia ya unyanyasaji mara nyingi hutokana na hali ngumu za utu, wivu na upungufu wa maadili. Watu wenye kutoa matusi na udhalilishaji kwa kawaida huwa na hali ya chini ya kujistahi, hali ya kujiona duni na kuhitajia kuangaliwa (kutizamwa) (6).
3. Tabia za utu wa wale wanaotukana wakubwa wa kidini
Kimsingi, watu ambao wanahusika katika hitilafu za kijamii kama vile udhalilishaji na matusi, wana historia ya utu iliyochochewa na ulioharibiwa, na wanahusika katika mashimo ya kina ya malezi ya kitamaduni na kijamii. Kwa mfano, tunataja baadhi yao:
3-1. Ukosefu wa utulivu wa kimaadili na kiroho
Watu wenye kutoa matusi na udhalilishaji kwa kawaida hawana mifumo imara ya kiadili na kiroho. Watu hawa wanatukana vitu vitakatifu vya uislamu kwa urahisi kwa sababu ya ule udhaifu wao waliokuwa nao katika elimu na malezi ya kidini(7).
3-2. Shakhsia zisizokuwa na uthabiti na zisizokuwa imara
Utafiti wa kisaikolojia umeonyesha kuwa watukanaji / wadhalilishaji wengi wana haiba au shakhsia isiyo na msimamo thabiti na matatizo ya kitabia. Watu hawa kwa kawaida hupambana na matatizo ya kifamilia, matatizo ya kiakili na matatizo ya kijamii(8).
3-3. Mchanganyiko wa ndani na hisia za unyonge
Watu wanaotukana na kudhalilisha wakubwa wa kidini mara nyingi hukabiliana na matatizo makubwa ya kisaikolojia na kijamii katika maisha yao ya kibinafsi. Kwa watu hawa, kutukana vitu vitakatifu vya kidini, kwao ni njia ya kutoa hasira zao na vinyongo vyao vya ndani(9).
4. Madhara ya kuwatukana wakubwa wa kidini
4-1. Athari za Kijamii na Kidini
Kutukana wwakubwa wa kidini kwa kawaida huambatana na mwitikio mkali (radiamali kali) kutoka kwa Waumini. Mfano wa hili ni mwitikio wa Waislamu - dhidi ya wale wenye - kumtukana na kumdhalilisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika miaka ya hivi karibuni(10).
4-2. Athari za Kihaki na Kikanuni (Kisheria)
Katika nchi nyingi, kuvunjia heshima matukufu ya kidini, inachukuliwa kuwa ni uhalifu. Katika jamii za Kiislamu, adhabu ya Kisheria inazingatiwa kwa uhalifu huu(11).
4-3. Athari za Kitamaduni na Maadili
Kutukana (kuwakosea adabu, kuwavunjia heshima) viongozi wakubwa wa kidini kunadhoofisha misingi ya maadili ya jamii na kueneza hali ya kutoaminiana. Tabia hizi zitasababisha polepole kuporomoka kwa maadili ya kitamaduni na kidini(12).
Kutukana viongozi wakubwa wa kidini ni jambo lenye mizizi mirefu yenye misukumo mbalimbali ya kisiasa, kiutamaduni na kisaikolojia.Tabia ya watu wanaotukana mambo matukufu ya kidini kawaida huhusishwa na udhaifu wa kimaadili, upungufu wa kisaikolojia na mambo ya ndani (ya nafsi zao).
(Radi amali au) Mwitikio wa Jamii za Kidini kwa matusi haya na udhalilishaji huu dhidi ya matukufu yao ya kidini, unaonyesha hadhi ya juu ya viongozi wakubwa wa kidini katika utamaduni wa Kiislamu. Ili kukabiliana na jambo hili, kunahitaji kuimarisha ujuzi wa kidini, kueneza zaidi mafundisho ya maadili, na kukabiliana (kushughulikia) na mambo yanayopingana na utamaduni.
-
Maelezo ya chini
1. Qur'an Tukufu, Surah Ahzab, Aya ya 56.
2. "Mitikio ya Waislamu kwa uchapishaji wa katuni za kukera (kuudhi)", Shirika la Habari la Farsi, 2022.
3. "Ukristo na udhalilishaji wa Matukufu ya Kidini", BBC Farsi, 2020.
4. Ibn Athir, al-kamal fi al-tarikh, Juzuu ya 4, uk 215.
5. Nasr Hamed Abu Zaid, Ukosoaji na utafiti juu ya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi, uk 45.
6. Fromm, Eric, Saikolojia ya udhalilishaji na Chuki, uk 110.
7. Chanzo kilichopita: Ukurasa wa 110.
8. Miller, James, Shakhsia zisizokuwa na uthabiti (imara), uk 73.
9. Freud, Sigmund, Uchambuzi wa Tabia za Kijamii, uk 88.
10. "Upinzani wa Waislamu kumtukana Mtume (SAWW)", Shirika la Habari la IRNA, 2022.
11. Kanuni ya Adhabu ya Kiislamu, Kifungu cha 513.
12. "Athari za udhalilishaji kwa jamii", gazeti la Kayhan, 2019.
Your Comment