Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ayatullah SayyId Sajid Ali Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Pakistan, akijibu matamshi ya matusi ya Rais wa Marekani kuhusu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah SayyId Ali Khamenei, alionyesha hali ya kutoridhika na kukemea vikali na kuonya kuwa: Matamshi kama haya ya jeuri yanaweza kusababisha athari mbaya ambazo sio tu kwamba haziwezi kuepukika, bali pia matokeo yake yatakuwa ya kutisha.
Amesema: "Ayatollah Al-Udhma, Sayyid Ali Khamenei si tu ni Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, bali pia ana nafasi nyeti na umuhimu wa kipekee miongoni mwa Umma wa Kiislamu na jamii ya Shia. Yeye ni shakhsia wa Kimataifa na anaheshimika katika ulimwengu wote wa Kiislamu."
Sajid Naqvi alisisitiza: "Mamlaka ya kiburi na uistikbari yanapaswa kutumia maneno ya heshima na yanayofaa, kwa kuzingatia adhama na msimamo wa shakhsia hao. Radiamali ya mamlaka za juu za Kimarjii na Wanazuoni Mashuhuri dhidi ya aina hii ya kauli (ya dharau ya Trump), inaashiria unyeti wa suala hilo, na inahofiwa kwamba kuendelea kwa uvunjifu huo wa heshima kutasababisha matukio ambayo matokeo yake yatakuwa machungu kwa kila mtu."
Mkuu wa Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Pakistan ameongeza kuwa: Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kusimama kidete na adhama yake, amewadhihirishia walimwengu kwamba yeye kamwe si mtu wa kuridhiana katika suala la hamasa na ghira ya Kiislamu na kulinda thamani na matukufu ya Kiislamu. Ayatollah Khamenei ametekeleza ipasavyo nafasi ya uongozi na uwakilishi wa ulimwengu wa Kiislamu, na kwa sababu hiyo amekuwa akipendwa na Waislamu kote ulimwenguni.
Your Comment