Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s), likiwa limejengwa juu ya itikadi ya kumwamini Imam Mahdi (a.t.f.s) aliyeahidiwa kwa mataifa yote, linabeba mafundisho yenye utajiri mkubwa kuhusu uadilifu na uokovu. Mafundisho haya yamewafanya Waislamu wa Kishia kubaki imara, thabiti na wenye heshima katika mitihani na misukosuko mikubwa ya ulimwengu wa Kiislamu.
Kuelewa mtindo wa maisha katika zama za sasa, ambazo ni zama za Ghaiba, ni swali muhimu. Kwa sababu kazi muhimu ni kuelimisha kizazi kinacholingana na zama za wahyi ili kumsaidia Imamu wa Zama (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na faraja yake). Kwa kuzichunguza kwa makini Aya na riwaya, kudhihiri na kuonekana kwa maisha mazuri na hatimaye kufikia maisha sahihi katika kipindi cha kudhihiri, kutadhihirika katika mwanga au kivuli cha elimu na marifa juu ya Hojja wa Mwenyezi Mungu.