Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesema kuwa lengo kuu la mashambulizi ya Israel dhidi ya Beirut ni kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Kishia nchini Lebanon na kubadili muundo wa kidemografia wa nchi hiyo. Amesisitiza kuwa Iran na Muqawama wa Lebanon ni washirika wa muda mrefu wanaosaidiana katika nyanja za kijeshi na kiutendaji.
Mkutano wa baadhi ya wapinzani wa kisiasa wa serikali ya Taliban ukiwa na kaulimbiu ya “Kuelekea Umoja na Uaminifu” umefanyika kwa siku mbili mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan. Katika mkutano huu, baadhi ya wasichana wa Shia, wakiwemo Zahra Joyaa, mwanahabari maarufu kutoka Afghanistan, pia walihudhuria.