Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema vita la hivi karibuni limeibua hitaji la kuainisha upya vipaumbele vya sekta ya ulinzi, huku uzalishaji wa baadhi ya vifaa vya kijeshi ukiongezeka hadi mara kadhaa licha ya vita.
Wizara ya Ulinzi na Msaada kwa Vikosi vya Iran imesisitiza kuwa, katika mazingira ya vita mseto na operesheni za kisaikolojia za maadui, waandishi wa habari wana jukumu muhimu katika kusimulia ukweli kwa uaminifu, kulinda maoni ya umma na kuimarisha uwezo wa kitaifa wa kuzuia vitisho.
"Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mkusanyiko wa damu zote zilizomwagika, subra, dhulma, mateso na juhudi za wanazuoni na Mashia katika historia nzima. Kuyaumiza mapinduzi haya ni sawa na kuumiza Uislamu kwa jeraha lisilopona kwa karne nyingi.”