Msimu wa mavuno ya mizeituni - ishara ya amani na ustawi kwa Wapalestina - umegeuzwa na utawala wa Kizayuni kuwa msimu wa hofu, damu na uharibifu.
Ukandamizaji na mashambulizi ya wakoloni wa Kizayuni yaongezeka kwa mpangilio na ukatili mkubwa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina, kupitia taarifa yake, imelaani vikali mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya raia wa Kipalestina na wanaharakati wa kigeni katika msimu wa kitaifa wa uvunaji wa zeituni katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.