Katika ziara ya Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (a.s) nchini Ivory Coast, alikutana kwa kifamilia na Kardinali Ignace Dogbo Assi, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini humo na mwakilishi wa Vatican. Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kidini, kuunga mkono heshima ya utu wa binadamu, na juhudi za kufanikisha amani ya kudumu duniani.
Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amemshitaki utawala wa Kizayuni wa Israel kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa na hukumu za Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICC), na kuhimiza hatua madhubuti kutoka kwa nchi za dunia ili kuzuia uhalifu unaoendelea wa utawala huo katika Ukanda wa Gaza.
Ametoa msisitizo kuwa mashambulizi yanayofanywa mara kwa mara na Israel dhidi ya raia wasio na hatia na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia, ni hali inayotakiwa kupokelewa kwa uzito mkubwa na jamii ya kimataifa.