Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amekutana na Spika wa Bunge la Iraq, Heibat Al-Halbousi, aliyefika Tehran akiwa na ujumbe wa wabunge kushiriki katika shughuli za maombolezo na kuaga kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Naibu Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Bagheri, amesema pendekezo la Iran la kuanzisha mfumo mpya wa usalama katika eneo limepokelewa vyema katika mkutano wa kimataifa wa viongozi wa usalama wa BRICS uliofanyika Moscow, huku akisisitiza umuhimu wa kuondoa ushawishi wa Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo.